Anjera Ya Kuku-By Rahime

Viungo
1.mayai matatu.
2.maziwa pakti moja.
3.uto kiasi.
4.maji kiasi.
5.unga ngano kilo moja.
6.kuku robo ama unavyojiskia.
7.sukari robo.
8.chumvi kiasi.

Namna ya kutayarisha.
Uchanganye unga, maziwa, sukari, chumvi kiasi, maji na mayai yako matatu.
Mchemshe kuku bila viungo vyovyote apate kuiva.
Kata kipande chako cha kuku katika vipande vidogovidogo.
Vitie vipande hivyo kwenye unga uchanganye vizuri.

Namna ya kupika.
Bandika chuma chako cha chapati kipate moto halafu itandaze unga ule wako mzito kiasi ili ijitokeze shepu ya mviringo.
Igeuze upande wa pili halafu uiache ipate kuiva na kuwa rangi ya maji kunde kiasi.
Upande huu utilie mafuta kiasi halafu ipike ka unavyopika chapati.

Ipo tayari.Epua na uendelee kupika mpaka unga wako uishe.
Iko tayari kuliwa kama snack tu ama ule na nyama kwa chai.

image

Author: salummy

Writers will always tell you about them through their pen....The power of the pen can transform hearts even a heart that has been plugged into darkness...

Share This Post On

5 Comments

  1. NYC meal n gud creativity ..lyk it

    Post a Reply
  2. Waaw nyc creativity..like it keep it up

    Post a Reply

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *